Shiriki na mchungaji rafiki.

BUILD 2021

Kongamano la Viongozi la Kimataifa kwa Njia ya Mtandao la BUILD 2021

Je, tunaijali hali ya Kanisa la leo? Je, tunawatamani watu wa Mungu na makuzi yao ya kiroho? Je, tunatamani kujenga juu ya ujumbe waliohubiri mitume wa kwanza?

Hili Kongamano ni kwa ajili ya kuwaandaa wachungaji na viongozi ili waweze kumtumikia Yesu vizuri zaidi katika kweli ya Neno la Mungu na uweza wa Roho Mtakatifu. Roho wa Mungu anatafuta watu, katika hizi siku za mwisho, ambao Mungu mwenyewe amewachagua kutoka kila pembe ya dunia, kushiriki katika kazi kubwa ya ujenzi wa Kanisa la Yesu Kristo

Mhubiri

Mchungaji Miki Hardy

Miki Hardy alikutana na Yesu na kuzaliwa mara ya pili mwaka 1977. Mapema tu alianza kuhisi wito wa Mungu maishani mwake akatumike. Alihamia Afrika Kusini ambapo alihudhuria chuo cha Biblia na akiwa huko ulitolewa unabii mwingi juu yake kutoka kwa Bwana kupitia watumishi wengi wa Mungu ambao hata hakuwafahamu, wakithibitisha wito alivyokuwa tangu alipookoka.

Baada ya muda alipitia kipindi kigumu sana maishani mwake na katika huduma yake. Katika kipindi hiki Bwana alishughulika kwa kina sana na moyo wake na akamfunulia ujumbe wa msalaba wa Yesu Kristo.

Ujumbe huu haukuacha moyo wake na, mwaka 2001, aliunda CTMI (Church Team Ministries International), Huduma ya Kimataifa ya Timu ya Kikanisa ambalo ni shirika la Kikristo linalolenga kuwawezesha na kuwaimarisha viongozi na makanisa barani Afrika na kwingineko kupitia ujumbe wa kitume wa msalaba. Katika kuyatimiza haya maono CTMI huandaa makongamano na mikutano mbalimbali, aidha hurusha mahubiri yake kwenye televisheni, redio, mitandaoni na njia nyinginezo za mawasiliano, barani Afrika na kwingineko ulimwenguni kote.

CTMI ni mtandao usiokuwa rasmi wa Kikristo ulioundwa mwaka 2001 na timu ya viongozi wa makanisa kutoka nchi mbalimbali ambao wameunganishwa na ujumbe wa msalaba na kazi ya Mungu maishani mwao. Maono ya CTMI ni viongozi na makanisa barani Afrika na kwingineko wawezeshwe na kuimarishwa kwa njia ya ujumbe wa kitume wa msalaba. www.ctmi.org Tovuti: www.ctmi.org